Cantitate/Preț
Produs

Kolonia Santita

Autor Enock Maregesi
Paperback – 12 sep 2012
'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya - na kung'oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifi a ya Magharibi - na duniani kwa jumla.
Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa Watanzania, Wakenya na Waganda - na jamii nzima ya Afrika ya Mashariki inayozungumza Kiswahili - na walowezi wa jamii yote ya Kiswahili duniani.
Citește tot Restrânge

Toate formatele și edițiile

Toate formatele și edițiile Preț Express
Paperback (1) 17919 lei  6-8 săpt.
  Authorhouse UK – 12 sep 2012 17919 lei  6-8 săpt.
Hardback (1) 29358 lei  6-8 săpt.
  Authorhouse UK – 13 sep 2012 29358 lei  6-8 săpt.

Preț: 17919 lei

Nou

Puncte Express: 269

Preț estimativ în valută:
3430 3528$ 2846£

Carte tipărită la comandă

Livrare economică 20 februarie-06 martie

Preluare comenzi: 021 569.72.76

Specificații

ISBN-13: 9781477222959
ISBN-10: 1477222952
Pagini: 406
Dimensiuni: 152 x 229 x 24 mm
Greutate: 0.66 kg
Editura: Authorhouse UK

Notă biografică

Enock Abiud Maregesi alizaliwa nchini Tanzania katika mkoa wa Mwanza mnamo mwaka 1972, Novemba 25. Alisomea teknolojia ya habari na utawala wa biashara katika Chuo Kikuu cha Wales, na uandishi wa habari na vitabu katika chuo cha fasihi ya ubunifu cha The Writers Bureau, nchini Uingereza. Alisomea pia sayansi ya roho ya Kabala katika Taasisi ya Bnei Baruch ya Petah Tikva nchini Israeli.
Mnamo mwaka 2015 kitabu chake cha kwanza, Kolonia Santita: Laana ya Panthera Tigrisi, kilishinda Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika; iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Cornell cha New York, Marekani, na kampuni ya Mabati Rolling Mills ya Nairobi nchini Kenya. Anaishi jijini Dar es Salaam, Tanzania, anakojishughulisha na biashara na uandishi wa vitabu.